Idris Sultan Amtundika Mimba Wema Sepetu

Mshindi wa Big Brother Afrika, Idris Sultan amepasua jipu kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu ambao umekuwa ukizua utata kila siku huku mashabiki wao wakiubatiza majina mbalimbali. Idris ameweka wazi kuhusu hali ya uhusiano wao na namna anavyomchukulia Wema Sepetu kama mkewe. Kwa mujibu wa maelezo yake, yeye na mrembo huyo wanatarajia kupata mtoto ingawa bado hawajafahamu jinsi ya..
Diamond Amwaga Machozi Ukumbini
Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo na kuwashangaza watu kufuatia mashabiki wake kumtaka awaimbie ‘akapela’ ya wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Tukio
hilo ambao bado limo midomoni mwa mashabiki wake, lilijiri usiku wa
kuamkia Boxing Day (Desemba 26, 2015) ndani ya ‘Uwanja wa Taifa wa
Burudani’ Dar Live jijini Dar ambapo nyota huyo alikuwa akikamua
jukwaani na shoo ya nguvu iliyopewa jina la Funga Mwaka Concert.
Dakika chache kabla Diamond hajamwaga chozi, mashabiki wake walimuomba aimbe ‘akapela’ ya wimbo huo mpya.
Wakati
akiimba akapela hiyo, mashabiki wake, bila kificho, walimwambia
anajitabiria ‘kufulia’ kwani wimbo huo una kila alama za yeye kumaliza
gemu la Bongo Fleva vibaya.
Hata
hivyo, licha ya mashabiki kumpasulia hivyo, baadhi yao walianza kulia
wakionekana kuguswa na mashairi ya wimbo huo hali iliyosababisha Diamond
naye aanze kulia na kushindwa kuendelea kuuimba wimbo huo.
Kufuatia
hali hiyo, dada yake kwa upande wa baba yake, Abdul Jumaa, Mwanahawa
Abdul ‘Queen Darleen’ alimfuata jukwaani na kumtoa huku akimfunika na
kitambaa cha bendera ya taifa ambacho pia dada huyo alikitumia kumfutia
machozi kaka yake huyo.
Diamond
alipelekwa nyuma ya jukwaa ambako ukiachia mbali yeye Queen Darleen,
meneja wake, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ naye alitumia nguvu ya ziada
kumbembeleza staa huyo huku akimwambia anawapa wasiwasi mashabiki wake.
Kwa hiyo anyamaze.
Licha
ya Babu Tale kutumia hekima ya kibabubabu, bado Diamond aliendelea
kulia, safari hii kwa uchungu zaidi na kujiinamia huku akikataa
kutulizwa wala kuambiwa maneno yoyote yanayoonekana ‘kama’ yana busara
ndani yake.
“Huna
sababu ya kuendelea kulia ndugu yangu kwani kufulia au kuendelea kuwa
na mali ni neema na msimamo wa Mungu. Hakuna binadamu anayeweza
kumshusha mwenzake kama Mungu hajapanga kuwa hivyo,” alisema Babu Tale lakini Diamond hakumsikiliza.
Diamond alinyamaza mwenyewe baadaye kufuatia mawasiliano ndani ya ubongo wake kumwambia ‘umelia sana kijana, imetosha sasa’!
Kilio
hicho, kilimaliza shoo hiyo kwani Diamond hakurudi tena jukwaani baada
ya kukamua nyimbo zake kibao na kuwafanya mashabiki wake kuiweka siku
hiyo katika kumbukumbu.
Wimbo ulimuliiza Diamond huu hapa
Wimbo ulimuliiza Diamond huu hapa
Mpekuzi blog
Kwa mashabiki wa Liverpool hizi sio habari njema kwa staa wao Daniel Sturridge …

Hizi haziwezi kuwa taarifa njema kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza anayeichezea klabu ya Liverpool Daniel Sturridge ambaye hakupata nafasi ya kucheza wala kukaa benchi katika mchezo wa michuano ya UEFA Europa League usiku wa November 26 dhidi ya Bordeaux katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield.
Staa huyo wa Liverpool
ambaye alikuwa nje ya uwanja toka October 4 baada ya kuwa majeruhi na
kulazimika kuwa nje ya kwa muda, alikuwa akitazamiwa kucheza mchezo wa Europa League usiku wa November 26 ila stori mpya ni kuwa nyota huyo ameshindwa kurejea uwanjani baada ya kuonekana bado alikuwa na tatizo.
Daniel Sturridge
mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikuwa akilalamika kuhisi maumivu
katika mguu wake, amepata nafasi ya kucheza mechi tatu pekee msimu huu
na 18 kwa mwaka 2015, alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli
3-2 dhidi ya Aston Villa September 26 lakini bado hajapata nafasi ya kucheza chini ya kocha mpya Jurgen Klopp.
Full Time ya Liverpool Vs Bordeaux Europa League Nov 26 2015

Usiku wa November 25 ilipigwa michezo ya mechi za klabu Bingwa barani Ulaya, lakini usiku wa November 26 ilikuwa ni zamu ya muendelezo wa mechi za michuano ya UEFA Europa League, klabu ya Liverpool ambayo inashiriki michuano hiyo ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Bordeaux katika dimba la Anfield.
Liverpool ambao wapo chini ya kocha wao mpya mjerumani Jurgen Klopp waliingia katika dimba lao la nyumbani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa goli 4-1 kutoka katika mchezo wao wa Ligi Kuu Uingereza iliyocheza dhidi ya Man City katika uwanja wa Etihad, Liverpool ilianza kwa kuruhusu kufungwa goli na Bordeaux dakika ya 33 kupitia kwa Henri Saivet.
Livepool ambao kwa muda
mrefu walikuwa wanaongoza kumiliki mpira, walifanikiwa kusawazisha goli
hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 38 kupitia kwa James Milner, Liverpool waliongeza mashambulizi na dakika ya 45 Christian Benteke akapachika goli la pili na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-1. Licha ya Bordeaux walionesha jitihada za kutaka kusawazisha goli kipindi cha pili, mchezo ulimazika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
No comments:
Post a Comment